WAFANYAKAZI WA SIDO WAHUDHURIA WARSHA YA FEDHA NA MIPANGO YA UPATIKANAJI WA NISHATI

Swahili

 

 

Wafanyakazi wa SIDO mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma waliweza kushiriki warsha ya fedha, mipango na upatikanaji wa nishati iliyoandaliwa na shirika la Practical Aid la Nchini Uingereza.Katika warsha hii waliweza kuangalia uhitaji wa teknolojia mbalimbali na uwezeshaji ambao utawezesha kufikia malengo ya kitaifa na dunia kwa ujumla.Uwezeshaji mbalimbali kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha ulijadiliwa kwa kushirikisha asasi za kiraia, taasisi binafsi na za kiserikali ili kufikia malengo.

Warsha hii ilijumuisha  wawakilishi wa Mikoa hiyo ambao ni Bwana Isaya Ndunguru( Afisa Mikopo-Rukwa),Bi Salome Charles(Afisa maendeleo ya biashara-Katavi) na Bwana Mabamba Majogoro( Meneja wa karakana-Kigoma) ilifanyika hoteli ya ziwa Tanganyika  tarehe 05 mwezi wa nne, 2018.