UJENZI WA MAENEO YA UZALISHAJI KWA WAJASIRIAMALI WAANZA MANYARA

Ili kuwawezesha wajasiriamali wa SIDO waweze kuzalisha bidhaa bora na salama, mchakato umeanza ambapo kila mkoa  itabidi utenge maeneo kwa ajili ya kujenga  majengo ambayo yatakuwa na mashine ambazo zitatumiwa na wajasiriamali watakaotaka kuzalisha bidhaa mbalimbali. Hii imetokana na changamoto wajasiriamali wengi walizonazo za kuwa na mtaji mdogo kwa ajili ya kujijengea kiwanda kulingana na taratibu zinavyotakiwa na hivyo kuwanyima fursa ya kupata alama za ubora.

Kutokana na utafutaji wa  wazabuni wa  ujenzi, SUMA JKT iliweza kushinda na hivyo kukabidhiwa kazi ya ujenzi kwenye mikoa ambayo ipo  tayari na ina maeneo kwa ajili ya ujenzi huo. Tukio la uzinduzi wa ujenzi katika eneo la SIDO Manyara limefuatia matukio kama hayo yaliyofanywa katika mikoa ya Simiyu, Geita, Kagera, Mtwara na Dodoma ambapo WaziriwaViwanda, BiasharanaUwekezaji (MB) mheshimiwa Charles Mwijage, alikabidhi eneo la Ekari 9 kwa SUMA JKT ambapo watajenga majengo (sheds) tatu (3) kwa ajili ya wajasiriamali.  

Pia ekari 3 zimejengwa ofisi za SIDO Mkoa. Hii itasaidia wajasiriamali ambao walikuwa wakifanya shughuli za uzalishaji katika maeneo ya makazi kupungua. Maombi mengi ya wajasiriamali wanaotaka kuanzisha viwanda yamepokelewa na SIDO Mkoa katika sekta za  Usindikaji wa Vyakula, Utengenezaji wa samani, Uchomeleaji vyuma, Utengenezajiwa sabuni, Utengenezajiwa chaki na  utengenezaji wa Bidhaa za ngozi.
Aidha Eneo hili ambalo litajengwa majengo litakuwa mkombozi kwa wajasiriamali, kwani wamekuwa na changamoto hiyo ya mahali pa kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango na kutanua wigo wa soko la bidhaa zao.