Shinyanga

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ni moja ya Halmashauri 5 zinazounda mkoa wa Shinyanga na ndio makao makuu ya Mkoa wa Shinyanga. Imepakana na Halmashauri ya Wilaya Shinyanga upande wa kaskazini, kaskazini magharibi,magharibi na kusini magharibi. Kuanzia upande wa mashariki hadi kusini mashariki imepakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ina jumla ya eneo ya kilometa za mraba 548. Eneo la utawala linaundwa na jumla ya tarafa 3, kata 17,vijiji 19, mitaa 25 na vitongoji 95.

Swahili
Subscribe to RSS - Shinyanga