Mpango Mkakati

MPANGO MKAKATI WA SHIRIKA  (CSP VI)  2017/18  HADI 2020/2021

1.1.   Msingi wa kutengenezwa kwake

              i.            Haja na uhitaji wa huduma za SIDO katika jamii,

            ii.      Mweleko wa wazi wa Serikali na Wadau kusaidia uhamasishaji wa maendeleo ya wajasiriamali wadogo,

          iii.            Uzoefu wa utoaji huduma uliopatikana,

          iv.            Changamoto zilizojitokeza,

            v.            Matokeo mazuri ya utekelezaji wa mipango makati iliyotangulia, na

          vi.            Fursa za uwekazaji na biashara zinazojitokeza

1.2.   Mpango huu unalenga:

        i.            Kuweka pamoja mafanikio yaliyopatikana, kutumia fursa mpya zinazojitokeza kuongeza ufanisi na tija kwa huduma zetu kwa wajasiriamali wadogo,

      ii.            Kuimarisha uwezo wa kitaasisi utakaiwezesha kutoa huduma nzuri na endelevu kwa wajasiriamali.

    iii.            Unaeleza wazi huduma zilizopo na uwezo wa shirika kuzitoa,

    iv.            Unahasisha kuongezeka ushiriki wa wadau katika kutoa huduma kwa wajasiriamali,

      v.            Kutoa mwelekeo na ishara kwa umma wa kile ambacho kimepangwa kwa ajili yao ili waweze kujiweka tayari kupata huduma husika.

1.3.   Dira:

Kuwa shirika linaloongoza katika kuendeleza viwanda/biashara nchini Tanzania kwa kuleta ufanisi na mafanikio kibiashara, huduma bora zinzofungua uwezekano wa ukuaji na ushindani katika sekta ya biashara ndogo mijini na vijijini.

1.4.   Dhamira:

Kuendeleza wajasiriamali wadogo kwa kuanzisha na kusaidia maendeleo ya tasnia ndogo na za kati za Viwanda na Biashara. Kipaumbele kinatolewa kwa Sekta ya uzalishaji inayochangia katika kuongeza kipato.

 

 

1.5.   HUDUMA NA PROGRAMU

1.5.1.                       KUWEZESHA WAJASIRIAMALI KUWA NA UBUNIFU,  UPATIKANAJI WA TEKNOLOJIA, MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA KIUFUNDI

 1. Wezesha wajasiriamali kupata teknolojia
 2. Jenga miundombinu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo
 3. Toa huduma za kuwaongezea uwezo mafundi stadi
 4. Hamasisha programu za ubunifu
 5. Hamasisha kuanzishwa kwa kongano za viwanda (kwa kutumia mfumo wa ODOP)

1.5.2.                       KUWEZESHA WAJASIRIMALI KUPATA UJUZI UTAKAOWAWEZESHA KUKUA NA KUHIMILI USHINDANI

 1. Programu za mafunzo kwa Wajasiriamali
 2. Wezesha kuanzisha na kuimarisha Ushirika/Vyama na Vikundi vya  ushirika wa wajasiriamali
 3. Kutoa huduma za uashauri wa kibiashara kwa wajasiriamali
 4. Tekeleza mkakati wa Wilaya Moja Bidhaa Moja (ODOP)
 5. Kuimarisha uwezo wa utoaji huduma wa ofisi za mikoa
 6. Kuimarisha uwezo wa utoaji huduma wa ofisi za mikoa

1.5.3.                       KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MASOKO  NA HABARI KWA WAJASIRIAMALI

 1. Tengeneza mkakati wa masoko na mawasiliano wa SIDO
 2. Kuongeza ufahamu na upatikanaji wa huduma za SIDO
 3. Ongeza uwezo wa wajasiriamali kushiriki katika masoko ya ndani na nje ya nchi
 4. Kutoa huduma za TEHAMA

1.5.4.                       KUWEZESHA WAJASIRIAMALI KUPATA HUDUMA ZA KIFEDHA

 1. Wajasiriamali kuimarishwa kwa kuwezeshwa kupata stadi na maarifa zihusianazo na huduma za kifedha
 2. Utoaji wa huduma za mikopo kwa wajasiriamali

1.5.5.                       KUIMARISHA UWEZO WA SHIRIKA KUFANYA KAZI

 1. Imarisha Nguvu Kazi ya Shirika
 2. Hakikisha upatikanaji wa nyenzo za kufundishia
 3. Huduma za udhibiti wa ndani, sheria, manunuzi na tathmini ya huduma zitolewazo.

Fungua Faili hapo chini kupata kablasha la Mpango kamili katika lugha ya Kiingereza

It appears your Web browser is not configured to display PDF files. Download adobe Acrobat