Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ni moja ya Halmashauri 5 zinazounda mkoa wa Shinyanga na ndio makao makuu ya Mkoa wa Shinyanga. Imepakana na Halmashauri ya Wilaya Shinyanga upande wa kaskazini, kaskazini magharibi,magharibi na kusini magharibi. Kuanzia upande wa mashariki hadi kusini mashariki imepakana na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ina jumla ya eneo ya kilometa za mraba 548. Eneo la utawala linaundwa na jumla ya tarafa 3, kata 17,vijiji 19, mitaa 25 na vitongoji 95.

Hali ya hewa ni ya kitropiki ambayo ina vipindi viwili ya majira ya mvua na kiangazi. msimu wa mvua ni kati ya mwezi Oktoba na Desemba,pia huanza mwezi machi hadi Mei. Kiasi cha mvua kwa mwaka ni kati ya milimita 600 hadi 1000. Kiangazi huanza mwezi Mei hadi Oktoba, pia huanza Januari hadi Februari. Watani wa jotoridi ni kati ya nyuzi za sentigredi 18 hadi 31.

Swahili
Sekta ya Huduma Inayotolewa: 
Mkoa: